
Ikiwa ni video ya nne ya rapper Young Killer, anasema ameboresha muonekano
wake na uchangamfu kwenye video yake, pia amefanya video hii na
director mpya kwenye tasnia ya video Tanzania akiamini kupata ubunifu
mpya. Humu yupo Young Killer ft Damian Soul- My Power na video
imeongozwa na Director Jackson Joachim, Audio ni kazi ya Mona Ganster wa
Classic Sound.